Tulijishughulisha na kila sekta baada ya kumaliza kidato cha nne nakumbuka hatukulupwa hata senti tano na mkuu wa shule Mwl Fast - Shule ya Msungi Munze Marieni Chome Same 1999
Nilipohitimu kidato cha nne nilienda Nyumba ya Mungu kufanya biashara ya maharage na kununua samaki kupeleka milimani 1999. Nilikua napenda sana raha hivyo nilienda kuogelea peke yangu kwenye dimbwi la ziwa ya Mungu niliogelea takribani kila siku ya week, sehemu niliyokua naogelea kulikua na mamba wengi ambao walikula mbuzi za wanyeji sana ila kwa bahati mbaya hakuna aliyeniambia na niliingiwa na mashaka kwanini watu wanaogelea mbali na si hapa ninapopapenda punde alitokea kijana mmoja jina lake anaitwa Emmanuel Mlacha aka Mhando, kwa kushangaa na kwa hofu kubwa aliniuliza wewe ni Mpare au Mnyamwanga nikamwambia mimi ni Mpare akaniambia toka haraka kwenye maji hapa ni hatari! Nikamwangalia nikataka kumwambia mbona umechelewa nimeoga wiki mbili hapa! Ila nikanyamaza tu akaniambia tumeshapoteza mbuzi watano mwaka huu na hapa natafuta mwingine nafikiri kaliwa. Nilitoka kwenye maji nikajiangalia nikasema sio kwa akili zangu wala nguvu zangu ila ni kwa Neema tu! Wewe unafikiri kwanini sijaliwa mpaka leo