2 years ago
936
15
Baada ya Ubelgiji kupoteza dira ya soka na kupotea kwenye ramani ya dunia ya mpira. Watu fulani walipewa kazi ya kurejesha makali ya Ubelgiji. Kilifanyika kikao fulani cha siri chini ya Mkurugenzi wa michezo Michael Sablon, wakachora mpango wa kuhakikisha Ubelgiji ya soka inarejea tena. Waliridhiana mambo mengi sana. Wakaweka na mpango wa namna ya kuutekeleza. Huo mpango ukaitwa 'MISSION 2006'. Tuombe uzima siku moja nitakuja kuulezea kipengele kwa kipengele🙏. Moja kati ya mkakati ulioanishwa siku ile, ni kutengeneza akademi nane za taifa zitakazosimamia vijana wanaoandaliwa kwa ajili ya taifa. Kutoka kwenye hizo akademi, wangechujwa wachezaji bora na kupelekwa kwenye akademi moja ya taifa, kutoka hapo wangepelekwa nje ya nchi. Katika kusuka zile akademi nane za taifa, hazikutengenezwa tu ilimradi. Ulifanyika utafiti wa kutambua sehemu ambazo vipo vipaji vingi kuliko maeneo mengine ya nchi. Akademi zikatengenezwa huko. Lipo jimbo moja zilitengenezwa akademi tatu. Si kwamba maeneo ambayo hayana vipaji vingi yalitelekezwa, bali nguvu iliwekwa maeneo yaliokuwa na vipaji vikubwa sana. Wale wa maeneo mengine wakakusanywa na kupelekwa nguvu ilipowekwa. Huu mkakati ndio uliwaleta kwenye ramani Axel Witsel, Mousa Dembele na Simon Mignolet. Kumbuka hiki ni kipengele kimoja tu ndani ya 'Mission 2006'. Picha ya vijana wawili wa Yanga Afrika hapo juu inafanya nini?? Msururu wa taifa lililosheheni wavulana wenye vipaji vikubwa vya soka, unahitaji mpango sahihi tu kuwavuna na kuwapata. Njia mojawapo ya kuwavuna ni kuwa na akademi KWELI za soka za kuwalea. Hauhitaji hata akademi nyingi, akademi chache tu kwenye maeneo yaliyosheheni vipaji vikubwa kuliko maeneo mengine. Kuwa na akademi chache itarahisisha ufuatiliaji na itarahisisha gharama, lakini pia itawapa vijana muda mrefu wa kuzoeana. Ubelgiji wana kizazi cha dhahabu kilichotengenezwa kwenye akademi nane tu za serikali. Kila mara ninapokatiza mitaa ya Morogoro na kuwatazama wanachokifanya wavulana wadogo wa shule wakiwa na mpira mguuni, nagundua kwanini wabelgiji walichagua kuweka nguvu kwenye baadhi ya maeneo. Nchi hii vipo vipaji vikubwa sana vya soka, MIPANGO tu.
Tempe wazo hili Rais wa nchi, ni msikivu na atatenda. Pia zaidi kwa wachezaji wakienda kucheza nje, kuna mapato makubwa sana ya kodi, kuanzia kuuzwa wachezaji, mishahara ya wachezaji n.k ambayo ingolstadt faida kubwa kwa nchi.
2 years ago
Acha kutudanganya unafk na umbea ungeandika kabla hata ya kucheza na simba sio baada ya mchezo ndio unatoa uchambuzi ulikuwa wapi kabla?????😂😂😂😂
2 years ago
Job💪💪💪
2 years ago